Litoka wapi ewe kifo?
Maswala ya kifo matata
Kwa hakika yana utata
Wazee na wadogo hata
Litoka wapi ewe kifo?
Meshindwa kukwelewa hasa
Kila kukicha watunyanyasa
Wapendwa kuwachukua bila ruhusa
Litoka wapi ewe kifo?
Mefanya wengi yatima
Huzuni manyumbani bila mama
Wajane mebaki kushika tama
Litoka wapi ewe kifo?
Njaa unayo ya ajabu
Hutosheki? Nipe jawabu
Ama angalau nipe sababu
Litoka wapi ewe kifo?
Machozi metuliza kwa asana
Twakusihi wapendwa wetu achana
Ewe adui wa milele amina
Litoka wapi ewe kifo?
Rudi kwa bwana wako iubilisi
Sikaribie tena achana nasi
Maishani mwetu huna nafasi
Ulikotoka ndio kwako kifo.