
Kansa au saratani
Gonjwa liwatishao wengi ulimwenguni
Jinamizi kuu lilozuka duniani
Litoka wapi gonjwa hili?
Gonjwa la rika zote
Halibagui jinsia laathiri zote
Halibagui kabila latuathiri sote
Litoka wapi gonjwa hili?
Mewageuza wengi mayatima
Yaua watoto,wazazi,jamii nzima
Mewaacha wengi kushika tama
Litoka wapi gonjwa hili?
Ila tusikate tamaa
Twaweza epuka balaa
Iwapo tutafanya inavyofaa
Tutaepuka gonjwa hili
Uvutaji wa sigara
Unywaji pombe kila mara
Vyote vyanzo vya madhara
Epuka uwe salama
Badili tabia na mienendo
Wingi wa matunda katika mlo ndio mtindo
Mazoezi kila mara uvivu kando
Uwe buheri wa siha
Tembelea vituo vya afya
Kila wakati uchunguzwe upya
Ikijulikana mapema itadhibitiwa
Uchunguzi wa saratani ni bure
Tushirikiane tuhamazishe jamii
Kuhusu athari za ugonjwa huu
Dalili na njia za kuudhibiti
Pamoja tuelimishane kama jamii
Saratani si utani
Mewauwa wengi mtaani
Ila tumechoka, sasa tumo vitani
Paza sauti za hamazisho nchini
Watu wapate kufahamu saratani
Sio gonjwa wastani
Fika leo hospitalini
Ufanyiwe uchunguzi
#PamojaTutashinda
#WeCancervive
Ungana nasi tarehe 4 mwezi huu katika kuhamazisha jamii kuhusu mbinu za kuudhibiti ugonjwa huu. Matembezi hayo yatafanyika mjini Eldoret. Usikose!