Viongozi wa upinzani

nawaomba kwa yakini

ajenda iwe ni amani

acheni ya uchochezi

 

za humu nchini siasa

mmejaza na mikasa

vurugu bungeni hasa

acheni ya uchochezi

 

Ughaibuni mkisafiri

zungumzeni kwa ari

nchi kuipa fahari

acheni ya uchochezi

 

Uamuzi wamahakama

ushafanyika hadi tama

ICC sasa mambo zama

acheni ya uchochezi

 

mmejawa na hekaya

kwa vyote mwaona ubaya

nauliza hamuoni haya?

Acheni ya uchochezi

 

Shida za hapa nchini

zatuhusu sote yakini

pamoja tuyatatue kwa amani

acheni ya uchochezi

 

serikali ina dosari tosha

zaweza zote kwisha

iwapo mtashiriki kusitisha

acheni ya uchochezi

 

tunapokaribia uchaguzi

enezeni amani na mapenzi

kwa wema mpate uongozi

acheni ya uchochezi

 

kwa pamoja mjenge Kenya

na serikali mwendeleze Kenya

bila chuki na tofauti Kenya

acheni ya uchochezi

 

Jina la Kenya la thamana

tuilinde tuienzi kwa sana

ukabila na ufisadi kupigana

acheni ya uchochezi

News Reporter
Emmanuel Yegon is an all-round communicator who is passionate about photography, poetry, broadcast journalism and digital strategy. He is committed to growth in the field of communication and best practice of journalism. Co-Founder and Communications Director ~ Mobile Journalism Africa www.mobilejournalism.co.ke