
Ubinadamu na utu
Wema mekosa kwa kila mtu
Mioyo watu mejaza kutu
Heri wanyama wa mwitu
Serikali mejaa wezi
Mashamba kuiba kila mwezi
Fedha kufuja ndio kazi
Ya vijana, walemavu na wazazi
Kuishi jiji kuu
Kweli utayaona makuu
Utapeli wa hali ya juu
Ama kweli ni mji mkuu
Askari wa baraza la jiji
Kuwahangaisha wauzaji
Watoa hukumu bila majaji
Eti wapate hongo-hitaji
Jiji megeuka shamba la wanyama
Sipostahimili talazimika kuhama
vurugu kila wakati hamna usalama
maovu mekua kawaida tazama
Taarifa zote mejaa utata
Viongozi kukicha wapigana vita
Meharibu dhana ya wakati wa Kenyatta
Kuwa Kenya hakuna matata
Ulimwengu umechanganyikiwa
Maovu yaendelea kusifiwa
Watu wema wadhulumiwa
Wengi bila hatia ovyo wauawa
Twahitaji badiliko la tabia
Tenda wema sipatikane na hatia
Kikosea omba msamaha pia
Tupendane, tuheshimiane pia