Tumuabudu Maulana
Hapa chini ulimwenguni
Kote kote makanisani
hata kule misikitini
Tumuabudu maulana
Hapa kwetu nchini
Hakika tumo taabani
Mna biashara makanisani
Tumuabudu maulana
Kila siku wahubiri
Tabia mbaya mekithiri
Sifa mbaya meshamiri
Tumuabudu maulana
Mewalaghai washiriki
Kuwapora bila haki
Hakika mbinguni hatufiki
Tumuabudu maulana
Hii leo makasisi
Megeuka waasi
Familia kufilisi
Tumuabudu maulana
Wake wa watu pia
Mewachukua waume walia
Wameshindwa kuvumilia
Tumuabudu maulana
Ufisadi hekaluni
Upinzani uongozini
Upotovu kwenye dini
Tumuabudu maulana
Mesababisha mauaji
Ya wengi waso wakosaji
Ila kwenu bora mtaji
Tumuabudu maulana
Mepotosha ibada
Mejipandisha lada
Mebadili mada
Tumuabudu maulana
Safari ya mbinguni
Tafadhali tubuni
Isigeuke ya kuzimuni
Tumuabudu maulana
Wokovu wa hakika
Hubirini bila wahka
Watu waje okoka
Tumuabudu maulana
Ili sote tuje patana
Mbinguni kukutana
Kwa furaha shikamana
Tukimuabudu maulana
i like the way u write your poems.. full of message. congrats
Reblogged this on yegonemmanuel8.