Usikate Tamaa
Usighubikwe na akilio
Bali tumaini la ufufuo
Likupe Amani moyoni
Kila jambo lina mwisho
Wapendwa kila kukicha
Waangamia bila mpango
Sife moyo ewe dada
Kila jambo lina mwisho
Hamna jema duniani
Ya hapa yote yapita
Ila jiandae ufae mbingu
Kila jambo lina mwisho
Tumaini hakika lipo
Maisha mema yapo huko
Akija mwokozi utakuwepo?
Kila jambo lina mwisho
Tuliza moyo ewe mpendwa
Msalabani mauti yalishindwa
Maisha ya milele tuliahidiwa
Kila jambo lina mwisho
Bado kitambo kidogo
Jiande kwa mwendo
Yesu yuaja upesi
Ndiye aliye na suluhisho