Kwa Yote Mlofanya
Mengi mawazo akilini
Ya muhimu kwa yakini
Makuu yalo nyumbani
Sitoyasahau maishani
Wa nne kwa kuzaliwa
Ndugu wengine sita sawa
Kwa maadili kulelewa
Kisomo hitaji kupewa
Nawashukuru sana wazazi
Kwa mema na makuu malezi
Baraka naomba kwa mwenyezi
Awape nafasi kwa yake enzi
Masomo kwa taabu metupa
Bila kazi karo kulipa
Zizini ng’ombe wote mehepa
Shamba pia hadi mekopa
Metufunza tabia njema
Uadilifu na heshima
Unyenyekevu na wema
Asanteni baba na mama
Umbali huu tumefika
Ni maulana hakika
Milele atatukuka
Jina lake Rabuka
Sasa mwachumia juani
Kuchanika kukicha kwa mpini
Twatia bidii masomoni
Ile mje kula kivulini
Msikat etamaa mungu yupo
Msichoke kamwe muombapo
Naamini mimi ila sio kiapo
Mema yaja tumaini lipo
Huenda leo twalia
Ugumu mwingi kupitia
Ila mola tukimkimbilia
Zigo atatua chozi tatufutia
Kwa: Baba, mama, na ndugu wote
Mungu awabariki