
Vyuo Vikuu Makao ya Makuu
Vyuo vyetu vikuu
Makao ya makuu
Kwa watakao ukuu
Twende pole kama wakuu
Visa na mikasa vyote
Kila kukicha kote kote
Utulivu twakosa sote
Twende pole kama wakuu
Vifo vingi kila mwaka
Wana nab inti tumezika
Uongozi wa kesho waadhirika
Twende pole kama wakuu
Siasa zetu mbovu
Zimejaa ukabila potovu
Zaendeleza mengi maovu
Twende pole kama wakuu
Tujiandae vema kwa mitihani
Tuifanye tukamilishe kwa Amani
Ila visababu vya kutofanya tusibuni
Twende pole kama wakuu
Maadili mezorota yakini
Mihadarati na uzinifu kiini
Mavazi mema hatutilii maanani
Twende pole kama wakuu
Vyombo vya habari zaonyesha
Migomo na vurugu tosha
Masomo na mitihani kusitisha
Twende pole kama wakuu
Viongozi wa kesho hasa
Wamo vyuoni wote sasa
Hivyo tujiepushe mikasa
Twende pole kama wakuu
Na tuwe bora mifano
Wa wema si mapambano
Kwa uridhiano na utangamano
Twende pole kama wakuu
Sote tu a kabila moja
La wakenya walo wamoja
Ukanila na chuki si haja
Twende pole kama wakuu
Kwa minajili ya wajukuu
Visasi vijavyo vyotr vikuu
Twenende vema tusikwae guu
Twende pole kama wakuu