Tukomeshe Ukeketaji

2
5214

Mimi ni mtoto msichana

Masomo kwangu ya maana

Ombi langu kwa jamii

Tukomeshe ukeketaji

 

Utamaduni huu wa zama

Watudhuru sana mama

Ombi langu kwa jamii

Tukomeshe ukeketaji

 

Napenda sana kusoma

Ili shida zipate kuhama

Ombi langu kwa jamii

Tukomeshe ukeketaji

 

Sihitaji kwa sasa kuozwa

Ila nafasi ya kusoma kutuzwa

Ombi langu kwa jamii

Tukomeshe ukeketaji

 

Hauna faida zozote

Ila taabu kwetu zote

Ombi langu kwa jamii

Tukomeshe ukeketaji

 

Ya kiafya madhara

Huja na nyingi hasara

Ombi langu kwa jamii

Tukomeshe ukeketaji

 

Ifikapo wakati wa uzazi

Twajawa na nyingi machozi

Ombi langu kwa jamii

Tukomeshe ukeketaji

 

Tukomeshe ukeketaji

Kikweli hatuuhitaji

Tusalie kikamilifu

Alivyokusudia muumbaji

2 COMMENTS

Comments are closed.