
”Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.- (Ufunuo 22:12-13)
Yuaja!
Ajira anao mkononi
Kwa wale wanaomwamini
Wanaomwabudu kwa roho na kweli
Wenye kustahimili kila hali
Washindao majaribu kwa imani
Wote watakua naye uzimani
Msife moyo!
Yatendeni yaliyo mema
Kila siku muwe wenye mienendo mema
Mkikosea ombeni msamaha
Mkikosewa pia mjifunze kusamehe
Kwa vyovyote wasaidieni wasojiweza
Kwa wote muwe vielelezo,mwangaza
Inukeni, angazeni!
Watangazie wote upendo
Utamaduni wa nyumbani upendo
Wajuze wote neno lake
Waite waje zizini pake
Wafanye wote wawe wanafunzi
Wamjie baba mungu mwenyezi
Yesu yuaja tena!
Mmejiandaa vipi kumpokea?
Mtakua wapi siku atakapotokea
Mawinguni kuja kuikomboa kanisa?
Jiandaeni leo,jiandaeni sasa
Msije Mkaachwa siku hiyo
Tumlaki bwana sote atakapokuja siku hiyo.
Bado kitambo Kidogo