
Tungekua na uwezo pengine tungechagua
Tungepata nafasi huenda tungeamua
Kwa kuzaliwa na kwa kuishi
Na majirani wa kuishi nao
Ila haya yote hatukuwa nayo
Tulizaliwa tukajipata tulipo
Rangi ya ngozi ni ile ile
Rangi nyekundu ya damu sawa
Tofauti zilitoka wapi?
Ila sote tu wanakenya
Binadamu wenye mioyo sawa
Kwenye mishipa damu yenye rangi sawa
Ukabila usitutenganishe hata!
Sote tu wana wa mungu
Tupendane ndugu wakenya
Tutangamane kwa Amani Kenya
Amani yahitajika kwa maendeleo
Siasa zisituvuruge, ni ya muda tu
Tufanye uchaguzi kwa Amani
Kisha tujenge nchi yetu pamoja
Kwa Amani, twende mbele bila chuki
Pamoja Tujenge Kenya
@yegonemmanuel_
https://www.facebook.com/theTribesSummit/